Yoshua 19:1 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 20021 Kura ya pili ilizipata ukoo za kabila la Simeoni na sehemu yao ya inchi ilikuwa imezungukwa na ile ya kabila la Yuda. အခန်းကိုကြည့်ပါ။ |
Kabila la Simeoni lilipata miji ya: Beri-Seba, Seba, Molada, Hasari-Suali, Bala, Ezemu, Eltoladi, Betuli, Horma, Ziklagi, Beti-Makaboti, Hasari-Susa, Beti-Lebaoti na Saruheni. Jumla ya miji waliyopewa ni kumi na mitatu pamoja na vijiji vyake. Vilevile kulikuwa miji ya Aini, Rimoni, Eteri, na Asani. Jumla ya miji mine pamoja na vijiji vyake, pamoja na vijiji vyote vilivyoizunguka miji hiyo mpaka Balati-Beri na Rama ya Negebu. Hiyo yote ni sehemu zilizopewa ukoo za kabila la Simeoni.