Lakini watu wa Yuda hawakuweza kuwafukuza Wayebusi, ambao ndio waliokuwa wenyeji wa Yerusalema, na mpaka leo Wayebusi wangali wanaishi katika muji ule pamoja na watu wa Yuda.
Waefuraimu hawakuwafukuza Wakanana walioishi Gezeri. Wakanana hao waliendelea kukaa kati ya watu wa Efuraimu mpaka leo, wakiwa watumwa wa kuwafanyia kazi za kulazimishwa.