Yoshua 15:20 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 200220-62 Hii ndiyo inchi watu wa kabila la Yuda waliyopewa kulingana na ukoo zake. Miji iliyokuwa upande wa kusini kabisa wa inchi ya Yuda kuelekea mupaka wa Edomu ilikuwa: Kabuseli, Ederi, Yaguri, Kina, Dimona, Adada, Kedesi, Hazori, Itinani, Zifu, Telemu, Bealoti, Hazori-Hadata, Kerioti-Hesironi (ni kusema Hazori), Amamu, Sema, Molada, Hazari-Gada, Hesimoni, Beti-Peleti, Hazari-Suali, Beri-Seba, Biziotia, Bala, Iyimu, Ezemi, Eltoladi, Kesili, Horma, Ziklagi, Madimana, Sanisana, Lebaoti, Silhimu, Aini na Rimoni. Jumla ya miji makumi mbili na tisa pamoja na vijiji vyake. Miji iliyokuwa kwenye mabonde ilikuwa: Estaoli, Zora, Asina, Zanoa, Eni-Ganimu, Tapua, Enamu, Yarmuti, Adulamu, Soko, Azeka, Sarayimu, Aditaimu, Gedera na Gederotaimu. Jumla ya miji kumi na mine pamoja na vijiji vyake. Zenani, Hadaza, Migidali-Gadi, Dilani, Misipe, Yokiteli, Lakisi, Bozikati, Eguloni, Kaboni, Lamani, Kitilisi, Gederoti, Beti-Dagoni, Nama na Makeda. Jumla ya miji kumi na sita pamoja na vijiji vyake. Libuna, Eteri, Asani, Ifita, Asina, Nesibu, Keila, Akizibu na Maresa. Jumla ya miji tisa pamoja na vijiji vyake. Ekuroni pamoja na miji yake midogo na vijiji, Miji yote na vijiji vilivyokuwa karibu na Asidodi kati ya Ekuroni na bahari, Asidodi na Gaza pamoja na miji na vijiji vyake, mpaka kijito cha Misri mpaka pembeni ya bahari ya Mediteranea. Miji iliyokuwa kwenye eneo la milima ni: Samiri, Yatiri, Soko, Dana, Kiriati-Sana (au Debiri), Anabu, Estemoa, Animu, Goseni, Holoni na Gilo. Jumla ya miji kumi na mumoja pamoja na vijiji vyake. Arabu, Duma, Esani, Yanimu, Beti-Tapua, Afeka, Humuta, Kiriati-Arba (au Hebroni) na Siori. Jumla ya miji tisa pamoja na vijiji vyake. Maoni, Karmeli, Zifu, Yuta, Yezereheli, Yokidamu, Zanoa, Kaina, Gibea na Timuna. Jumla ya miji kumi pamoja na vijiji vyake. Halihuli, Beti-Zuri, Gedori, Marati, Beti-Anoti na Eltekoni. Jumla ya miji sita pamoja na vijiji vyake. Kiriati-Bali, unaoitwa tena Kiriati-Yearimu, na Raba. Jumla ya miji miwili pamoja na vijiji vyake. Miji ya jangwa ilikuwa: Beti-Araba, Midini, Sekaka, Nibusani, Muji wa Chumvi na Engedi. Jumla ya miji sita pamoja na vijiji vyake. အခန်းကိုကြည့်ပါ။ |