Lakini sasa amekufa, kwa nini nifunge? Mimi ninaweza kumurudisha katika dunia? Siku moja, nitakwenda kule alikokwenda, lakini yeye hawezi kurudi kwangu.”
Sisi wote tutakufa. Sisi ni kama maji yaliyomwangika chini ambayo hayawezi kuzoleka. Lakini Mungu hataki Abusaloma akufe sasa au aendelee kuishi mbali naye.
Usikie maombi yangu, ee Yawe, usikilize kilio changu, usikae kimya ninapolia. Maana, mimi ni kama mugeni tu anayepita, ni musafiri kama vile babu zangu wote walivyokuwa.