2 Heri uchungu wangu ungepimwa, nayo mateso yangu yote yangewekwa katika mizani!
Hata leo malalamiko yangu ni ya uchungu. Ninapata maumivu na kuugua.
Lakini sasa shida imekupata nawe unaregea. Imekugusa, nawe unafazaika.
Yobu akamujibu Elifasi:
Moyo unajua uchungu wake wenyewe, wala mugeni hawezi kushiriki furaha yake.