21 Wewe unapaswa kujua, wewe ambaye umekwisha ishi miaka mingi!
Wewe ndiwe mutu wa kwanza kuzaliwa? Wewe ulizaliwa mbele ya kuwa kwa vilima?
Yobu, tangu uzaliwe umekwisha kuamuru kupambazuke na kufanya mapambazuko yajue pahali pake,
Umekwisha kuingia katika akiba za teluji, au kuona akiba za mvua ya mawe
Ulikuwa wapi nilipoiweka misingi ya dunia? Uniambie, kama una maarifa.