Hiyo ni siku ya giza na huzuni; siku ya mawingu na giza nene. Jeshi kubwa linakaribia kama giza linalofunikia milima. Namna hiyo haijapata kuwa hata kidogo wala haitaonekana tena katika vizazi vyote vinavyokuja.
Malaika wa tano akamwanga kikombe chake juu ya kiti cha kifalme cha yule nyama wa ajabu, na ufalme wake ukafunikwa na giza. Watu wakaanza kutafuna ndimi zao kwa sababu ya maumivu.