23 Kwa nini kumujalia uzima mutu ambaye njia zake zimefungwa, mutu ambaye Mungu amemwekea kizuizi?
Akibomoa, hakuna anayeweza kujenga upya; akifunga mutu, hakuna anayeweza kumufungua.
Unanifunga minyororo kwenye miguu, unachunguza njia zangu zote, umeichapa miguu yangu.
Majeshi yake yananifikia kwa pamoja; yametengeneza njia ya kuja kwangu, yamepiga kambi kuizunguka nyumba yangu.
Mujue kwamba Mungu amenitendea vibaya na kuninasa katika wavu wake.
Njia yangu ameiziba kwa ukuta kusudi nisipite, njia zangu amezitia giza.
Mutu kama yule atashangilia sana na kufurahi atakapokufa na kuzikwa!
Nitashangilia na kufurahia wema wako, maana wewe unaona taabu yangu, unajua huzuni yangu.
Hasira yako imenilemea; umenisonga kwa zoruba yako yote.
Umewafanya warafiki zangu waniepuke, umenifanya kuwa chukizo kwao. Nimefungwa wala siwezi kutoroka.
Enyi watu wa Israeli wazao wa Yakobo, kwa nini munalalamika na kusema: Yawe hatujali sisi! Mungu wetu hajali haki yetu!
Amenizungushiia ukuta na siwezi kutoka, amenifunga kwa minyororo mizito.
Amezifunga njia zangu kwa mawe makubwa, amepotosha mapito yangu.
Na watoto wake sitawahurumia, maana ni watoto wa uzinzi.