1 Yobu akaendelea kutoa masemi yake, akasema:
Masemi yenu ni mezali za majivu, maneno yenu ni ukuta wa udongo.
Kisha Yobu akaendelea na masemi yake, akasema:
Maneno yangu ni mazitomazito; mawazo yangu ni ya hekima.
Nitasema nanyi kwa mafumbo, nitasema mambo yaliyofichwa tangu zamani;
Mezali katika midomo ya mupumbafu ni kama miguu ya kiwete inayoninginia.
Balamu akamutolea Balaki mashairi yake, akasema: Balaki amenileta hapa kutoka Aramu, hakika, mufalme wa Moabu amenileta kutoka milima ya mashariki: Kuja uwalaani watu wa Yakobo kwa ajili yangu, hakika, kuja uwakaripie Waisraeli!
Basi, Balamu akasema mashairi haya: Mashairi yangu mimi Balamu mwana wa Beori, mashairi ya mutu aliyefumbuliwa macho,
naye akasema mashairi haya ya Yawe: Mashairi yangu mimi Balamu mwana wa Peori mashairi ya mutu aliyefumbuliwa macho.