Ni nani aliyepanda juu mbinguni na kushuka chini? Ni nani aliyekamata upepo katika mukono? Ni nani aliyefunga maji katika kitambaa? Ni nani aliyeweka mipaka yote ya dunia? Jina lake ni nani? Na ni nani jina la mwana wake? Uniambie kama unajua!
Nitalifanya ukiwa kabisa, mizabibu yake haitasafishwa matawi wala kupaliliwa. Litaota michongoma na miiba. Tena nitayaamuru mawingu yasinyeshe mvua juu yake.
Anapotoa sauti, maji yananguruma katika mbingu, anapandisha mawingu toka kwa miisho ya dunia. Anaufanya umeme upige wakati wa mvua, na kuuvumisha upepo katika gala zake.