7 Macho yangu yamefifia kwa ajili ya uchungu; viungo vyangu vyote vimekuwa kama kivuli.
Macho yangu ni mekundu kwa sababu ya kulia, kope zangu zimekuwa nyeusi sana,
Warafiki zangu wanizarau; ninatoa machozi kumwomba Mungu.
Amenifanya ninyauke na huo ni ushuhuda juu yangu. Kukonda kwangu kumenishitaki na kushuhudia juu yangu.
Mwili wangu umejaa vidudu na uchafu; ngozi yangu imekauka na kutokwa na usaha wa jipu.
Ninatoweka kama kivuli cha magaribi; nimepeperushwa kama nzige.
Ninatabanika kwa kulia kwa uchungu; usiku ninalowanisha kitanda changu kwa machozi; kwa kulia kwangu ninalowanisha matandiko yangu.
Macho yangu yamechoka kwa huzuni; yamefifia kwa kutaabishwa na waadui.
Nani anayejua yanayofaa kwa mutu katika maisha haya mafupi yasiyokuwa na faida, maisha ambayo yanapita kama kivuli? Nani anayejua yale yatakayotukia chini ya jua nyuma ya kufa kwake?
Kwa ajili ya hiyo tumeugua ndani ya moyo, kwa ajili ya hiyo macho yetu yamefifia.