7 Kweli Mungu amenichakalisha, ameharibu kila kitu karibu nami.
Ninachukia maisha yangu! Malalamiko yangu nitayasema bila kizuizi. Nitasema kwa uchungu wa moyo wangu.
Warafiki zangu wanizarau; ninatoa machozi kumwomba Mungu.
Mungu amewaweka wandugu zangu mbali nami; warafiki zangu wakubwa wamenitoroka kabisa.
Kule kwa wafu waovu hawasumbui mutu, kule wanaochoka wanapumzika.
Kweli kwangu hakuna kitu cha kunisaidia; musaada wowote ni mbali nami.
Ninayachukia maisha yangu. Sitaishi milele. Muniache, maana siku zangu ni pumzi tu!
Basi nimepangiwa miezi na miezi ya taabu, urizi wangu ni kuteseka usiku kwa usiku.
Bwana wetu Yawe amenifundisha jinsi ya kusema, kusudi niwatie moyo wale waliochoka. Kila asubui ananipa hamu ya kusikiliza mambo anayotaka kunifundisha.
Kwa hiyo nami, nimeanza kuwaangusha chini, na kuwaangamiza kwa sababu ya zambi zenu.