6 Lakini nikisema maumivu yangu hayatulii, na nikikaa kimya hayaondoki.
Ninachukia maisha yangu! Malalamiko yangu nitayasema bila kizuizi. Nitasema kwa uchungu wa moyo wangu.
Ningeweza kuwatia moyo kwa maneno yangu, na maneno yangu ya faraja yangewatuliza.
Ninasema: “Nitasahau malalamiko yangu, niondoe uso wangu wa huzuni na kuwa na furaha!”
Lakini ninaogopa maumivu yangu yote, maana ninajua Mungu hataniona kuwa sina kosa.