8 Mikono yako ilinitengeneza na kuniumba, lakini sasa unageuka kwa kuniangamiza.
Ni sawa kwako kunionea, kuzarau kazi ya mikono yako na kupendelea mipango ya waovu?
Nani atakayebishana nami? Niko tayari kunyamaza na kufa.
Kweli! Ninajua utanipeleka tu katika kifo, pahali wote wanaoishi watakapokutana.
Yeye ananiponda kwa zoruba, anaongeza vidonda vyangu bila sababu.
Yote ni mamoja, kwa hiyo ninasema: Mungu anawaangamiza wakamilifu na waovu.
Mujue kwamba Yawe ndiye Mungu. Yeye ndiye aliyetuumba, sisi ni mali yake; sisi ni watu wake na kondoo wake anaowachunga.
Kwa mikono yako wewe mwenyewe uliniumba; unijalie akili nijifunze amri zako.
Ee Yawe, utatimiza yote uliyoniahidia. Wema wako, ee Yawe, unadumu milele. Usisahau kazi ya mukono wako mwenyewe.
Umbo langu halikufichikwa kwako nilipoumbwa kwa uficho, nilipotengenezwa ndani ya tumbo la mama yangu.
Wewe uliniona hata mbele sijazaliwa. Uliandika kila kitu katika kitabu chako; siku zangu zote ulizipanga, hata mbele hakujakuwa ile ya kwanza.
Yeye anaunda mioyo ya watu wote, yeye anajua kila kitu wanachofanya.
Kila mumoja anajulikana kwa jina langu; niliwaumba wote na kuwafanya kwa ajili ya utukufu wangu.”