Kwa hiyo simba kutoka pori atawaua; imbwa wa pori kutoka jangwa atawararua. Chui anaivizia miji yao. Kila mutu anayetoka humo atararuliwa vipandevipande, kwa sababu zambi zao ni nyingi, maasi yao ni makubwa.
Maana mimi nitakuwa kama simba kwa Efuraimu, kama simba mukali kwa watu wa Yuda. Mimi mwenyewe nitawararua na kuondoka, nitawakamata na hakuna atakayewaokoa.