11 Uliuumba mwili wangu kwa mifupa na mishipa, ukaifunika mifupa yangu kwa nyama na ngozi.
Si wewe uliyenimimia kama maziwa, na kunigandisha kama siagi?
Ukanipa uzima na kunitendea mema, ukalinda nafsi yangu kwa uangalifu.
Wewe uliniumba mwili wangu wote; ulinitengeneza katika tumbo la mama yangu.
Kwa uongozi wake, viungo vyote vya mwili vinashikamana kabisa, nao mwili wote muzima unashikamana vizuri kwa nguvu ya maunganio yake. Halafu, kila kiungo kinapotumika kama kinavyopaswa, mwili wote unakomaa na kujijenga katika upendo.