Katika siku zile Yesu akasema: “Ee Baba, Mwenyeji wa mbingu na dunia, ninakushukuru kwa maana mambo uliyoyaficha kwa watu wenye hekima na elimu, umeyafunua kwa wanaokuwa wadogo.
Hata hivi wengi kati ya wakubwa wa Wayuda wakamwamini Yesu. Lakini kwa sababu ya Wafarisayo, hawakushuhudia kwamba wameamini. Waliogopa kwamba watatengwa wasiingie katika nyumba ya kuabudia.