66 Basi kwa sababu ya maneno haya, wengi kati ya wanafunzi wake wakamwacha, nao hawakutembea tena pamoja naye.
Nitawaangamiza wote walioniacha mimi Yawe, wote walioacha kunitafuta na kuniuliza shauri.
Lakini yule kijana aliposikia maneno hayo, akajiendea akihuzunika, kwa sababu alikuwa tajiri sana.
Lakini Yesu akamujibu: “Mutu yeyote anayeanza kulima na kuanza tena kuangalia nyuma hafai kutumika katika Ufalme wa Mungu.”
Yesu alialikwa vilevile kwenye ndoa ile pamoja na wanafunzi wake.
Wengi kati ya wanafunzi wake waliposikia maneno haya, wakasema: “Masemi haya ni magumu. Ni nani anayeweza kuyakubali?”
Lakini kuna wengine kati yenu wasioamini.” (Yesu alisema vile kwa sababu alijua tangu mwanzo wale wasioamini na yule atakayemutoa.)
wandugu za Yesu wakamwambia: “Ondoka hapa, uende Yudea kusudi wanafunzi wako waone matendo unayofanya.
Basi Yesu akawaambia wale Wayuda waliomwamini: “Kama mukitii mafundisho yangu, ninyi ni wanafunzi wangu hakika.
Kama unavyojua wewe mwenyewe, watu wote wa jimbo la Azia wameniacha; kati yao kuna Figelo na Hermogene.
Dema amependelea mambo ya dunia hii akaniacha na kwenda Tesalonika. Kreske akaenda Galatia, na Tito akaenda Dalmatia.
Mwenye haki mbele yangu ataishi kwa njia ya imani. Lakini kama akirudi nyuma, sitapendezwa naye.”
Watu hawa wametoka kati yetu, lakini hawakukuwa wa kundi letu, na kwa sababu hii wametuacha. Kama wangekuwa wa kundi letu, wangekaa pamoja nasi. Lakini wametuacha kusudi ionekane wazi ya kama hawakukuwa wa kundi letu.