Yesu Kristo ndiye aliyekuja kwa maji ya ubatizo wake na kwa damu ya kufa kwake. Hakukuja na maji tu, lakini pamoja na maji na damu. Naye Roho ndiye anayeshuhudia mambo yale kwa sababu Roho ni wa ukweli.
Watu wote wameshuhudia Demetrio vizuri; hakika ukweli wenyewe unahakikisha jambo lile. Sisi vilevile tunamushuhudia, nawe unajua kwamba ushuhuda wetu ni wa kweli.