vilevile akaona kitambaa kilichofunika kichwa cha Yesu. Kitambaa kile hakikuwekwa pamoja na vile vingine, lakini kilikuwa kimekunjwa na kuwekwa peke yake pahali pengine.
Halafu mwanafunzi yule aliyependwa na Yesu akamwambia Petro: “Ni Bwana.” Simoni Petro aliposikia kwamba ni Bwana, akavaa kanzu yake (kwa maana alikuwa havai kitu), naye akajitupa ndani ya maji.