14 Alipokwisha kusema maneno haya, akageuka nyuma, akamwona Yesu akisimama pale, lakini hakutambua kwamba ni yeye.
Ingawa Yosefu aliwatambua kaka zake, wao hawakumutambua.
Mara moja Yesu akakutana na wale wanawake, akawasalimia. Wakajongea karibu naye, wakamushika miguu na kumwabudu.
Kisha, Yesu akawatokea wanafunzi wawili, akiwa na sura ingine. Wanafunzi hao walikuwa wanakwenda kwenye vijiji.
Yesu alipokwisha kufufuka asubui mapema, siku ya kwanza ya juma, alimutokea kwanza Maria wa Magdala, yule aliyefukuza pepo saba toka ndani yake.
lakini macho yao yalizuizwa kumutambua.
Halafu, macho yao yakafumbuliwa, wakamutambua. Lakini yeye akatoweka, nao hawakumwona tena.
Lakini yeye akapita katikati yao, na kujiendea.
Asubui mapema, Yesu akaonekana kandokando ya ziwa, lakini wanafunzi hawakutambua kwamba ni yeye.
Kwa ajili ya hii, wakaokota mawe kwa kumutupia. Lakini Yesu akajificha na kutoka ndani ya hekalu.