Wataniomba wakuwe wengi kama kundi la kondoo wa kutolewa sadaka, kama kundi la kondoo katika Yerusalema wakati wa sikukuu zake. Hivi ndivyo miji yenu iliyokuwa ukiwa itakavyojaa makundi ya watu. Kwa hiyo watatambua kwamba mimi ni Yawe.
Kisha wakafika Yerusalema. Yesu alipoingia ndani ya hekalu, akaanza kufukuza watu waliokuwa wakiuzishia na kununulia vitu vyao ndani ya hekalu. Akapindua meza za wale waliobadilisha feza na viti vya wachuuzi wa njiwa.
Kisha akawafundisha maneno haya: “Imeandikwa katika Maandiko Matakatifu: ‘Nyumba yangu itaitwa nyumba ya maombi kwa mataifa yote.’ Lakini ninyi mumeigeuza kuwa nafasi ya kukutania ya wanyanganyi!”
Basi akasokota kamba kuwa fimbo na kuwafukuza wote toka hekalu pamoja na kondoo na ngombe wao. Kisha akapindua meza za wenye kubadilisha feza na kuzimwanga chini.