Yesu akaingia ndani ya hekalu, naye akawafukuza watu wote waliokuwa wakiuzishia na kununulia vitu vyao ndani yake. Akapindua meza za wale waliobadilisha feza na viti vya wachuuzi wa njiwa.
Kisha wakafika Yerusalema. Yesu alipoingia ndani ya hekalu, akaanza kufukuza watu waliokuwa wakiuzishia na kununulia vitu vyao ndani ya hekalu. Akapindua meza za wale waliobadilisha feza na viti vya wachuuzi wa njiwa.
Kulikuwa kumebaki siku moja mbele ya kutimia kwa sikukuu ya Pasaka. Yesu alijua kwamba saa yake ya kutoka katika dunia na kurudi kwa Baba yake imetimia. Yeye alikuwa akiwapenda watu wake waliokuwa katika dunia, na akaendelea kuwapenda mpaka mwisho.
“Wanaume wote wa taifa lenu watakuja mbele ya Yawe, Mungu wenu, mara tatu kila mwaka, pahali ambapo Yawe, Mungu wenu atachagua: wakati wa sikukuu ya Pasaka, sikukuu ya kuvuna na wakati wa sikukuu ya vibanda. Wasitokee mbele ya Yawe mikono mitupu.