Ubaguzi wao unashuhudia juu yao; wanatangaza zambi yao kama vile watu wa Sodoma, wala hawaifichi. Ole kwao watu hao, kwa sababu wamejiletea maangamizi wenyewe.
Walisikia haya walipotenda machukizo hayo? Hapana, hawakusikia haya hata kidogo. Hata zamiri hazikuwagonga. Kwa hiyo, wataanguka pamoja na wale walioanguka; nitakapowaazibu, wataangamia. –Ni Yawe anayesema hivyo.