14 Mimi nimetangaza neno lako kwao, na dunia imewachukia kwa sababu wao si wa dunia, kama vile mimi nisivyokuwa wa dunia.
Nitaweka uadui kati yako na yule mwanamuke, kati ya uzao wako na uzao wake. Yeye ataponda kichwa chako, nawe utamwuma kisigino chake.”
Mwovu ni chukizo kwa mwenye haki, naye mwenye haki ni chukizo kwa mwovu.
Kwa muda wa mwezi mumoja, nikaua wachungaji watatu wabaya. Tena uvumilivu wangu kwa kondoo ukaniishia, nao kwa upande wao, wakanichukia.
Nao wakamujibu: “Tunaweza.” Yesu akaongeza kuwaambia: “Hakika mutakunywa kikombe nitakachokunywa, na kubatizwa kama vile nitakavyobatizwa.
Wao si wa dunia, kama vile mimi nisivyokuwa wa dunia.
kwa maana nimewatangazia maneno yale uliyoniagiza, nao wameyakubali. Wamejua hakika kwamba nilitoka kwako na kuamini kwamba wewe ndiwe uliyenituma.
Watu wa dunia hawawezi kuwachukia ninyi, lakini wananichukia mimi kwa sababu ninashuhudia kwamba matendo yao ni mabaya.
Yesu akawajibu: “Ninyi munatoka hapa chini, lakini mimi nimetoka juu. Ninyi ni wa dunia hii, lakini mimi si wa dunia hii.
Tusikuwe kama Kaina aliyekuwa wa yule Mwovu, akamwua ndugu yake. Yeye alimwua kwa sababu gani? Kwa sababu matendo yake yalikuwa mabaya na ya ndugu yake yalikuwa ya haki.
Basi wandugu zangu, musishangae kama watu wa dunia hii wakiwachukia ninyi.