Yoane 11:44 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002
44 Halafu yule marehemu akatoka inje, akiwa amefungwa mikono na miguu kwa vitambaa, na uso wake ukifunikwa na nguo. Yesu akawaambia: “Mumufungue, mumwache ajiendee.”
Inanipasa kuwakomboa hawa watu kutoka kuzimu; sharti niwaokoe kutoka kifo! Ewe kifo, mapigo yako ni wapi? Ewe kuzimu, kuangamiza kwako ni wapi? Mimi sitawaonea tena huruma!
Yesu akasema: “Muondoshe jiwe hili!” Marta, dada wa yule marehemu, akamujibu: “Bwana, anaanza sasa kunuka, kwa maana ni siku ine sasa tangu alipozikwa!”
vilevile akaona kitambaa kilichofunika kichwa cha Yesu. Kitambaa kile hakikuwekwa pamoja na vile vingine, lakini kilikuwa kimekunjwa na kuwekwa peke yake pahali pengine.
Yeye atabadilisha huu mwili wetu wa uzaifu na kuufananisha na mwili wake wa utukufu kwa nguvu ambayo kwa njia yake anaweza kuwa na mamlaka juu ya vitu vyote.