30 (Yesu alikuwa hajaingia bado katika kijiji, alikuwa angali pahali Marta alipomukuta.)
Marta aliposikia kama Yesu anakuja, akaenda kumupokea katika njia, lakini Maria alibaki ndani ya nyumba.
Marta alipokwisha kusema maneno hayo, akaenda kumwita dada yake Maria na kumwambia kwa siri: “Mwalimu amekuja, na anakuita.”
Wakati Maria aliposikia hivi, akaondoka upesi kwenda kumukuta.