Bwana wetu Yawe atakiangamiza kifo milele! Atayafuta machozi katika nyuso za watu wote na kuondoa haya ya watu wake katika dunia yote. Yawe amesema hivyo.
Wafu wako wataishi tena, miili yao itafufuka. Wanaolala katika mavumbi wataamuka na kuimba kwa furaha! Mungu atapeleka umande wake wa uzima, nao wanaokuwa kwa wafu watatoka wazima.
Inanipasa kuwakomboa hawa watu kutoka kuzimu; sharti niwaokoe kutoka kifo! Ewe kifo, mapigo yako ni wapi? Ewe kuzimu, kuangamiza kwako ni wapi? Mimi sitawaonea tena huruma!
Kwa njia ya imani, wanawake wamoja walifufuliwa na kurudishiwa wale waliofiwa nao. Wengine waliteswa mpaka kufa, nao wakikataa kuachiliwa kusudi wapate ufufuko unaokuwa bora zaidi.