Mumutukuze Yawe, Mungu wenu, mbele hajawaletea giza, mbele hamujajikwaa miguu kwenye milima inayofunikwa na giza. Ninyi mulitazamia mwangaza, lakini anaugeuza kuwa usiku anaufanya kuwa giza nzito.
Lakini wewe Yawe uko pamoja nami. Kwangu wewe ni kama shujaa wa kutisha. Kwa hiyo watesaji wangu watajikwaa, nao hawataweza kunishinda. Watafezeheka kabisa, kwa sababu hawatashinda. Haya yao itadumu hata milele, nayo haitasahauliwa.
Lakini halizami ndani yao kama mizizi. Wanalishika kwa muda mufupi tu. Wakati taabu na mateso vinapowafikia kwa ajili ya Neno la Mungu, mara moja, wanaanguka.