Moyo wangu unaugua kwa ajili ya inchi ya Moabu; wakimbizi wake wanakimbilia Zoari, wanakimbia mpaka Egilati-Selisiya. Wanapanda njia ya kwenda Luhiti wakilia, katika njia kwenda Horonaimu wanatoa kilio cha maangamizi.
ni kama joto la jua juu ya inchi kavu. Lakini wewe unakomesha fujo ya wageni. Kama wingu linavyofifisha joto la jua, ndivyo unavyokomesha nyimbo za ushindi za watu wakali.