Matawi ya miti yamekauka na kuvunjika; wanawake wanayaokota na kuyawasha moto. Watu hawa hawajaelewa kitu, kwa hiyo Mungu, Muumba wao, hatawahurumia, yeye aliyewafanya, hatawatendea mema.
Yawe anasema: Watu wangu ni wapumbafu, hawanijui mimi. Wao ni watoto wajinga; hawana ufahamu. Wao wanaelewa vizuri kutenda maovu, lakini hawajui kutenda mema.
Watu wangu wameangamia kwa kutonijua, maana wewe kuhani umekataa mafundisho. Nimekukataa kuwa kuhani wangu. Kwa maana umeisahau sheria ya Mungu wako, nami vilevile nitawasahau watoto wako.
vipofu wanapata kuona, viwete wanatembea, wenye ukoma wanatakaswa, viziwi wanapata kusikia, wafu wanafufuliwa na Habari Njema inahubiriwa kwa wamasikini.