Basi, Yona akasimama kwa kukimbilia Tarsisi, mbali na uso wa Yawe. Akaenda mpaka katika muji wa Yofa ambapo alikuta mashua moja iko tayari kwenda Tarsisi. Alilipa bei ya safari, akapanda ndani ya mashua, akasafiri pamoja na watu wengine kwenda Tarsisi, mbali na uso wa Yawe.