“Ee Yawe, ninakusihi ukumbuke jinsi nilivyokutumikia kwa uaminifu na kwa moyo wangu wote na kutenda mazuri mbele yako.” Hezekia akalia kwa uchungu sana.
Ninajua, Mungu wangu, kwamba wewe unapima moyo, nawe unapendezwa na uaminifu. Nami, katika uaminifu wa moyo wangu nimetoa vitu hivi vyote kwa mapenzi yangu, na sasa ninaona watu wako wanaokuwa hapa, wakikutolea kwa mapenzi yao na furaha.
Nami nikasema: Lakini wewe Yawe unanielewa vizuri; unikumbuke na kuja kunisaidia. Unilipizie watesaji wangu kisasi. Wewe ni muvumilivu, usiniache niangamie; kumbuka kwamba ninatukaniwa kwa ajili yako.
Uwapatishe haya wale wanaonitesa, lakini usiniache mimi kupata haya. Uwafezeheshe watu hao, lakini usiniache mimi kufezeheka. Uwaletee ile siku ya hasara, uwaangamize kabisakabisa!
Kisha Yesu akamwuliza mara ya tatu: “Simoni mwana wa Yoane, unanipenda?” Basi Petro akauzika kwa sababu Yesu alimwuliza mara ya tatu kama anamupenda. Kwa hiyo akamujibu: “Bwana, unajua yote; unajua kama ninakupenda!” Yesu akamwambia: “Tunza kondoo wangu.
Walimu hawa wa uongo ni kama nyama wasiokuwa na akili ambao wanazaliwa tu kwa kunaswa na kuchinjwa. Wao wanasema vibaya juu ya mambo yote wasiyojua. Wataangamizwa kufuatana na ubaya wao wenyewe.