Kisha mufalme akasimama kwa pahali pake akafanya agano mbele ya Yawe, kumufuata Yawe, kushika amri, maamuzi na masharti yake kwa moyo wake wote na kwa roho yake yote, kutenda maneno yote ya agano yaliyoandikwa katika kitabu hiki.
Yawe akaniambia: Tangaza maneno hayo yote katika miji ya Yuda na katika barabara za Yerusalema. Uwaambie watu wayasikilize masharti ya agano hili na kuyashika.