Katikati ya miungu ya uongo ya mataifa nani anayeweza kunyesha mvua? Au, ni mbingu ndiyo inaweza kutoa manyunyu? Si ni wewe ee Yawe, Mungu wetu? Tunakuwekea wewe tumaini letu, maana ni wewe unayefanya haya yote.
Ingawa vile hakuacha kujijulisha kwa njia ya kutenda mema. Anawanyeshea mvua toka mbingu, anawapa mavuno kwa wakati wake, anawapa chakula na kuwajaza na furaha.”