Biblia Todo Logo
အွန်လိုင်း သမ္မာကျမ်းစာ

- ကြော်ငြာတွေ -




Waroma 4:9 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002

9 Uheri huu si kwa watu wanaotahiriwa tu, lakini ni kwa watu wasiotahiriwa vilevile. Kwa maana tumekwisha kusema kwamba Abrahamu alihesabiwa kuwa mwenye haki kwa njia ya imani yake.

အခန်းကိုကြည့်ပါ။ ကော်ပီ




Waroma 4:9
14 ပူးပေါင်းရင်းမြစ်များ  

Abramu alimwamini Yawe, naye Yawe akamuhesabu kuwa mwenye haki.


Yeye anasema: Haitoshi tu wewe kuwa mutumishi wangu, kusudi uyainue makabila ya Yakobo, na kurudisha watu wa Israeli waliobaki. Nitakufanya ukuwe mwangaza wa mataifa, kusudi watu wote wapate kuokolewa katika dunia.


Ndio utakaowaangazia mataifa, na kuleta utukufu kwa watu wako Waisraeli.”


Yeye alihesabiwa vile alipokuwa katika hali gani? Alipokuwa amekwisha kutahiriwa au alipokuwa hajatahiriwa bado? Halikutendeka nyuma ya kutahiriwa kwa Abrahamu lakini mbele ya kutahiriwa kwake!


Kwa maana Maandiko Matakatifu yanasema: “Abrahamu alimwamini Mungu na kwa hiyo akahesabiwa kuwa mwenye haki.”


Ilitendeka hivi kusudi kwa njia ya Yesu Kristo, baraka Mungu aliyoahidi kwa Abrahamu itolewe vilevile kwa watu wa mataifa mengine na hata sisi kwa njia ya imani, tupate kupokea yule Roho aliyeahidiwa na Mungu.


Mimi ni mudogo kuliko watu wote wa Mungu, lakini Mungu amenijalia neema ya kutangaza kwa watu wa mataifa mengine Habari Njema ya baraka za Kristo zisizoweza kuhesabiwa.


Kwa hiyo hakuna tena tofauti kati ya watu wa mataifa mengine na Wayuda, wenye kutahiriwa na wasiotahiriwa, wageni, washenzi, watumwa na watu huru. Lakini Kristo ni yote naye yuko katika wote.


ကြှနျုပျတို့နောကျလိုကျပါ:

ကြော်ငြာတွေ


ကြော်ငြာတွေ