Solomono alipomaliza maombi yake, moto ukashuka kutoka mbinguni na kuchoma sadaka na sadaka za kuteketeza kwa moto zilizotolewa, kisha utukufu wa Yawe ukajaza nyumba.
Wakati Haruni alipokuwa akizungumuza na Waisraeli wote pamoja, watu wote wakaangalia kule katika jangwa na mara moja utukufu wa Yawe ukaonekana katika mawingu.
ngombe dume mumoja na kondoo dume mumoja kwa ajili ya sadaka ya amani, wamutolee Yawe sadaka pamoja na sadaka ya unga uliochanganywa na mafuta kwa maana leo Yawe atawatokea.
Naye Kora akawakusanya watu wote pamoja, wakasimama mbele ya Musa na Haruni ambao walikuwa kwenye mulango wa hema la mukutano. Halafu utukufu wa Yawe ukawatokea watu wote.