Feza zilizotolewa kwa sadaka za malipo kwa ajili ya kosa na kwa sadaka za usamehe wa zambi hazikuingizwa katika nyumba ya Yawe. Hizo zilikuwa ni mali ya makuhani.
Basi, kuhani atamufanyia yule mutu ibada ya upatanisho kwa ajili ya zambi, naye atasamehewa. Unga unaobaki utakuwa wa kuhani kama vile inavyofanyika juu ya sadaka ya ngano.
Kati ya vitu vitakatifu kabisa ambavyo haviteketezwi kwa moto, hivi vitakuwa vyenu: sadaka za vyakula, sadaka kwa ajili ya zambi na sadaka za kosa. Kila kitu watu watakachonitolea kama vile sadaka takatifu kitakuwa chako na wana wako.
Munajua hakika kuwa wale wanaotumika katika hekalu wanapata chakula chao ndani ya hekalu. Na wale wanaotumika kwa kutoa sadaka juu ya mazabahu wanapata sehemu yao kutoka sadaka zile.