Feza zilizotolewa kwa sadaka za malipo kwa ajili ya kosa na kwa sadaka za usamehe wa zambi hazikuingizwa katika nyumba ya Yawe. Hizo zilikuwa ni mali ya makuhani.
Kisha atachinja yule mwana-kondoo katika Pahali Patakatifu, wanapochinjia nyama wa sadaka kwa ajili ya zambi na sadaka ya kuteketezwa kwa moto. Sadaka hii kwa ajili ya kosa na vilevile sadaka kwa ajili ya zambi, ni mali ya kuhani. Ni sadaka takatifu kabisa.
Lakini ikiwa mutu huyo amekufa na hana ndugu wa karibu ambaye anaweza kupokea malipo hayo, basi, malipo ya kosa yatatolewa kwa Yawe kwa ajili ya makuhani; malipo haya ni pamoja na kondoo dume wa upatanisho ambaye atatumiwa kwa kumufanyia upatanisho kwa ajili ya zambi yake.
Munajua hakika kuwa wale wanaotumika katika hekalu wanapata chakula chao ndani ya hekalu. Na wale wanaotumika kwa kutoa sadaka juu ya mazabahu wanapata sehemu yao kutoka sadaka zile.