Yule mutu akaniambia: Vyumba hivi vyote ni vitakatifu. Ndani ya vyumba hivi makuhani wanaoingia mbele ya Yawe, wanakula sadaka takatifu kabisa: sadaka takatifu kabisa na humo ndimo munamowekwa sadaka za vyakula, sadaka za kuomba kusamehewa zambi na sadaka kwa ajili ya malipo ya kosa kwa sababu pahali hapo ni patakatifu.