Wazao wa Haruni wataiteketeza juu ya mazabahu pamoja na sadaka ya kuteketezwa inayokuwa juu ya kuni. Hiyo ni sadaka ya kuteketezwa kwa moto yenye harufu nzuri ya kumupendeza Yawe.
Yawe akamwambia Haruni: Ninakupatia matoleo Waisraeli waliyonipa, vitu vyote vitakatifu walivyonipa: vitu vyote vilivyotakaswa na Waisraeli. Ninakupa vitu vyote wewe na wazao wako kuwa fungu lenu, na hiyo ni haki yenu milele.
Kisha kuhani atatwaa bega la yule kondoo dume likiwa limepikwa pamoja na andazi moja lililotiwa chachu kutoka kikapu na mikate myembamba vilevile isiyotiwa chachu na kumupa munaziri katika mikono akisha kumaliza kunyoa nywele zake alizokuwa nazo wakati wa kutakaswa.