Walawi 7:16 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002
16 Lakini kama sadaka hiyo ya amani ni ya kutimiza kiapo au ya mapenzi mema, itakuliwa siku hiyohiyo inapotolewa na sehemu ingine inaweza kukuliwa kesho yake.
Waisraeli wote, wanaume na wanawake, ambao walivutwa ndani ya moyo wao kuleta kitu chochote kwa ajili ya kazi ambayo Yawe alikuwa amemwagiza Musa ifanyike, walileta vitu hivyo kwa mapenzi yao, kama vile muchango wa kumupa Yawe.
Mufalme anapotaka kumutolea Yawe sadaka kwa mapenzi yake, ikiwa ni sadaka ya kuteketezwa au sadaka ya amani, watamufungulia mulango wa kiwanja cha ndani unaoelekea upande wa mashariki. Atatoa sadaka kama anavyofanya siku ya Sabato, na anapotoka, mulango ufungwe nyuma yake.
Ngombe dume au mwana-kondoo anayekuwa na kiungo kimoja kirefu au kifupi kuliko kawaida wanaweza kumutoa sadaka ya mapenzi. Lakini huyo usimutoe kuwa sadaka ya kutimiza kiapo.
Sadaka hizo ni pamoja na zile munazonitolea mimi Yawe siku ya Sabato kama vile na sadaka zenu za kawaida, sadaka za kutimiza viapo vyenu, na sadaka zenu za mapenzi munazonitolea mimi Yawe.
mukinitolea mimi Yawe sadaka kutoka katika mifugo yenu, sadaka ya kuteketezwa au sadaka ya kutimiza kiapo au kutoa sadaka ya mapenzi au sadaka ya wakati wa sikukuu zenu zilizowekwa, na kufanya harufu nzuri ya kunipendeza mimi Yawe,
basi huko pahali Yawe, Mungu wenu, atakapochagua kusudi jina lake likae pale, hapo mutapeleka yote ninayowaamuru: sadaka zenu za kuteketeza kwa moto na sadaka zingine, sehemu ya kumi za mazao yenu, na sadaka za kutimiza kiapo.
Musikule vitu hivi pahali munapoishi: sehemu ya kumi za ngano zenu, divai zenu au mafuta yenu, wazaliwa wa kwanza wa ngombe wenu au kondoo wenu, au sadaka zenu za kutimiza kiapo au za mapenzi, au matoleo mengine.
Vilevile huko mutapeleka sadaka zenu za kuteketezwa kwa moto na sadaka zingine, sehemu ya kumi za mazao yenu, matoleo yenu ya mapenzi na ya kutimiza kiapo, na wazaliwa wa kwanza wa ngombe na kondoo wenu.