Halafu Hezekia akawaambia watu: “Sasa mumekwisha kujitakasa, mukaribie, mulete sadaka na matoleo ya shukrani katika nyumba ya Yawe.” Basi, watu wakaleta sadaka zao na matoleo yao ya shukrani, na za kuteketeza.
Akarudisha mazabahu ya kumwabudia Yawe, na juu yake akatoa sadaka za amani na za shukrani, akawaamuru watu wa inchi ya Yuda wamwabudu Yawe, Mungu wa Israeli.
Watatoa kondoo mumoja kwa kila kundi la kondoo mia mbili katika jamaa za Waisraeli. Wataleta sadaka za vyakula, sadaka za kuteketezwa kwa moto, na sadaka za amani, kusudi wapate kufanyiwa upatanisho. –Ni ujumbe wa Bwana wetu Yawe.–
Hata mukinitolea sadaka zenu za kuteketezwa kwa moto na za vyakula, mimi sitakubali kuzipokea; na sadaka zenu za amani za nyama wanono mimi sitaziangalia kabisa.