Kore mwana wa Imuna, Mulawi, aliyekuwa mulinzi wa Mulango wa Mashariki wa hekalu, akasimamia matoleo yote ya mapenzi kwa Mungu; na kugawanya matoleo kwa ajili ya Yawe na sadaka zinazokuwa takatifu kabisa.
Halafu katika baraza karibu na njia kulikuwa meza mbili upande mumoja na zingine mbili upande mwingine. Meza hizo zilitumika kuwa pahali pa kuchinjia sadaka ya kuteketezwa, sadaka ya usamehe wa zambi na sadaka ya malipo ya kosa.
akaniambia hivi: Hapa ndipo makuhani watakapopikia nyama ya sadaka ya malipo ya kosa, sadaka ya kusamehewa zambi, na kupika sadaka za vyakula. Kwa hiyo hawatoki inje ya baraza na chochote, kusudi watu wasijichafue kwa kugusa kitu kitakatifu.
Ikiwa hawezi kutoa hua wawili au vitoto viwili vya njiwa kama vile sadaka yake kwa ajili ya zambi aliyotenda, basi, ataleta unga kilo moja. Lakini hatautia mafuta wala ubani maana ni sadaka kwa ajili ya zambi.
Kama mutu yeyote akikosa kwa kutenda zambi bila kujua juu ya kutokutoa vitu vitakatifu Yawe anavyotolewa, atamuletea kondoo dume asiyekuwa na kilema kutoka kundi lake. Wewe utapima bei yake kulingana na kipimo cha Pahali Patakatifu. Hiyo ni sadaka kwa ajili ya kosa.
Lakini kama hawezi kutoa mwana-kondoo wa sadaka ya kosa kwa ajili ya zambi aliyotenda, basi atamuletea Yawe hua wawili au vitoto viwili vya njiwa, mumoja kwa ajili ya sadaka ya zambi na mwingine kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa kwa moto.
na kujitakasa kwa Yawe kwa siku zake za kujitenga. Hizo siku za kwanza hazitahesabiwa kwa sababu nywele zake zilizokuwa zimetakaswa zimechafuka. Atatoa mwana-kondoo dume wa mwaka mumoja kuwa sadaka ya kosa.