Walawi 6:20 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002
20 Chochote kitakachogusa nyama hiyo kitakuwa kitakatifu. Nguo yoyote ikidondokewa na damu ya sadaka hiyo, basi, nguo hiyo itafuliwa katika Pahali Patakatifu.
Pamoja na hayo, walisaidia katika kazi kutayarisha mikate mitakatifu, unga safi na sadaka ya vyakula, maandazi yasiyotiwa chachu, sadaka ya mikate iliyokaangwa, sadaka ya mikate iliyochanganywa na mafuta, na sadaka katika kazi ya upimaji wa wingi wa sadaka na ukubwa wake.
mikate isiyotiwa chachu, maandazi yasiyotiwa chachu yaliyopondwa kwa mafuta, na mikate myembamba isiyotiwa chachu, lakini iliyopakwa mafuta. Vyote hivi vikuwe vimetengenezwa kwa unga laini wa ngano.
Pamoja na sadaka hiyo, mutatoa sadaka ya vyakula ya kilo mbili za unga laini uliochanganywa na mafuta ambayo mutanitolea mimi Yawe kwa moto, na harufu yake itanipendeza. Sadaka yake ya kinywaji ni litre moja ya divai.
Kama mutu yeyote akitakiwa kutoa ushuhuda kwenye baraza juu ya jambo aliloona au kusikia naye akikataa kusema kitu, basi, huo ni uovu na atabeba azabu ya zambi ile.
Ikiwa hawezi kutoa hua wawili au vitoto viwili vya njiwa kama vile sadaka yake kwa ajili ya zambi aliyotenda, basi, ataleta unga kilo moja. Lakini hatautia mafuta wala ubani maana ni sadaka kwa ajili ya zambi.
Wazao wanaume wa Haruni ndio peke yao wanaoruhusiwa kula sehemu hiyo maana hiyo imetengwa siku zote kwa ajili yao kutoka sadaka Yawe anazotolewa kwa moto. Yeyote atakayezigusa atakuwa mutakatifu.
Uwaambie kwamba sadaka watakayonitolea ya kuteketezwa kwa moto, itakuwa hii: wana-kondoo wawili wa mwaka mumoja wasiokuwa na kilema chochote, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa ya kila siku.
Eleazari mwana wa kuhani Haruni atatunza mafuta ya taa, ubani wa kufukiza, sadaka za vyakula za kila siku, mafuta ya kupakaa kwa kutakasa na kila kitu kilichotakaswa katika hema hilo.
Yeye hahitaji kutoa sadaka kila siku kama vile Makuhani wengine Wakubwa, kwanza kwa ajili ya zambi zake mwenyewe na kisha kwa ajili ya zambi za watu. Kwa maana amefanya vile mara moja tu wakati alipojitoa mwenyewe kufa.