Nikaagiza matoleo ya kuni kufanyika katika wakati unaopaswa na malimbuko wakati wake. Ee Mungu wangu, unikumbuke kwa ajili ya haya yote na unijalie mema.
na chumba kinachoelekea upande wa kaskazini ni kwa ajili ya makuhani wanaotumika kwenye mazabahu. Makuhani hawa ni wale wa ukoo wa Zadoki, ndio hao kati ya watu wa kabila la Lawi wanaoruhusiwa kwenda mbele ya Yawe.
Wazao wanaume wa Haruni ndio peke yao wanaoruhusiwa kula sehemu hiyo maana hiyo imetengwa siku zote kwa ajili yao kutoka sadaka Yawe anazotolewa kwa moto. Yeyote atakayezigusa atakuwa mutakatifu.
Tangu wakati wa kutakaswa kwa Haruni na wazao wake wanapaswa kumutolea Yawe kilo moja ya unga laini kwa siku, nusu moja ya unga huo ataitoa asubui na nusu ingine magaribi.
Yawe akawasha moto ukaiteketeza sadaka ya kuteketezwa na mafuta yaliyokuwa juu ya mazabahu. Watu wote walipoona huo moto wakapiga vigelegele na kuinama uso mpaka chini.