Biblia Todo Logo
အွန်လိုင်း သမ္မာကျမ်းစာ

- ကြော်ငြာတွေ -




Walawi 6:11 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002

11 Wazao wanaume wa Haruni ndio peke yao wanaoruhusiwa kula sehemu hiyo maana hiyo imetengwa siku zote kwa ajili yao kutoka sadaka Yawe anazotolewa kwa moto. Yeyote atakayezigusa atakuwa mutakatifu.

အခန်းကိုကြည့်ပါ။ ကော်ပီ




Walawi 6:11
14 ပူးပေါင်းရင်းမြစ်များ  

Kwa siku saba utafanyia mazabahu upatanisho na kuitakasa. Nyuma ya hayo, mazabahu itakuwa takatifu kabisa na chochote kitakachoigusa kitakuwa kitakatifu.


Watakapotoka kwenda kwenye kiwanja cha inje kwa watu, watatosha nguo walizovaa wakati walipokuwa wanatumika na kuziweka katika vyumba vitakatifu. Ni lazima wavae nguo zingine, kusudi watu wasijitakase kwa kugusa nguo zao.


Yule ngombe dume na mbuzi waliotolewa sadaka kwa ajili ya zambi ambao damu yao ilipelekwa katika Pahali Patakatifu kwa kufanya ibada ya upatanisho, watapelekwa inje ya kambi na kuteketezwa kwa moto. Ngozi zao, nyama na mavi yao, vyote vitateketezwa kwa moto.


Haruni na wazao wake peke yao ndio wanaoruhusiwa kula mikate hiyo maana ni mitakatifu kabisa kwa sababu ni sehemu ya sadaka ninazotolewa mimi Yawe kwa moto. Hiyo ni haki yao milele.


ni kusema ngombe muzima aliyebakia atamupeleka na kumuteketeza inje ya kambi pahali safi ambapo majivu yanatupwa, naye atamuchoma kwa moto juu ya kuni. Atachomwa kwa moto pale pahali pa kumwangia majivu.


Kisha atamutwaa ngombe dume huyu na kumupeleka inje ya kambi na kumuteketeza kwa moto kama vile alivyofanya yule mwingine. Hiyo ni sadaka kwa ajili ya zambi ya jamii.


Usipikwe hata kidogo pamoja na chachu. Nimewapa wao sehemu hiyo kutoka sadaka wanazonitolea kwa moto. Ni sadaka takatifu kabisa kama vile sadaka kwa ajili ya zambi na kwa ajili ya kosa zinavyokuwa.


Chochote kitakachogusa nyama hiyo kitakuwa kitakatifu. Nguo yoyote ikidondokewa na damu ya sadaka hiyo, basi, nguo hiyo itafuliwa katika Pahali Patakatifu.


Wanaoruhusiwa kuikula ni wanaume wa ukoo wa makuhani peke yao kwa vile hiyo ni sadaka takatifu kabisa.


Wanaoruhusiwa kula sadaka hiyo ni wanaume wa ukoo wa makuhani peke yao; ni sadaka takatifu kabisa. Itakuliwa katika Pahali Patakatifu.


ကြှနျုပျတို့နောကျလိုကျပါ:

ကြော်ငြာတွေ


ကြော်ငြာတွေ