Kisha utatwaa mafuta ya yule kondoo dume: mukia wake, mafuta yanayofunika matumbotumbo na sehemu bora ya maini, figo zake mbili na mafuta yake, pamoja na paja la kuume. (Kondoo yule ni kondoo wa utakaso.)
Wazao wa Haruni wataiteketeza juu ya mazabahu pamoja na sadaka ya kuteketezwa inayokuwa juu ya kuni. Hiyo ni sadaka ya kuteketezwa kwa moto yenye harufu nzuri ya kumupendeza Yawe.
Kisha, akatwaa mafuta yote yaliyokuwa kwenye matumbotumbo yake, sehemu bora ya maini pamoja na figo zote mbili na mafuta yake na kuviteketeza juu ya mazabahu.
Kisha, akatwaa mafuta yote, mukia pamoja na mafuta yake, mafuta yote yanayofunika matumbotumbo, sehemu bora ya maini, pamoja na figo zote mbili, mafuta yake na paja la muguu wa kuume wa nyuma wa huyo kondoo dume.