Mbali na wingi wa sadaka za kuteketeza, kulikuwa vilevile mafuta ya sadaka ya amani, hata kulikuwa sadaka ya kinywaji kwa ajili ya kila sadaka za kuteketeza. Hivyo basi, kazi za ibada zikaanzishwa tena katika hekalu.
Mafuta yote ya mbuzi huyo atayaondoa kama vile anavyoondoa mafuta ya nyama wa sadaka ya amani, naye kuhani atayateketeza juu ya mazabahu, na harufu yake nzuri itamupendeza Yawe. Basi, kuhani atamufanyia yule mutu hiyo ibada ya upatanisho, naye atasamehewa.