Yule kijana ambaye mama yake aliitwa Selemoti binti ya Dibri wa kabila la Dani, alitukana Mungu na kuzarau jina lake. Basi watu wakamupeleka kijana kwa Musa,
Haruni na wazao wake peke yao ndio wanaoruhusiwa kula mikate hiyo maana ni mitakatifu kabisa kwa sababu ni sehemu ya sadaka ninazotolewa mimi Yawe kwa moto. Hiyo ni haki yao milele.
Kati ya Waisraeli kulikuwa kundi fulani lililoandamana nao ambalo lilikuwa na hamu kubwa ya kula nyama. Waisraeli wenyewe wakalia, wakisema: Heri kama tungeweza kupata nyama ya kula!